Kuhusu e-Kijumbe

e-Kijumbe ni mfumo wa kidigitali unaowawezesha watu kuchangiana hela kwa ratiba ya mzunguko kupitia tovuti rasmi www.ekijumbe.xyz. Mfumo huu umejengwa kwa misingi ya usalama, uwazi, na nidhamu.

Uanachama huanza kwa kujisajili na kulipia ada, ambapo mwanachama hujiunga na kikundi kulingana na uwezo wake. Mfumo huendesha michango ya mzunguko kwa haki kwa kila mwanachama, huku ukihifadhi historia, kutoa taarifa, na kurahisisha mikopo ya ndani.

🌍 Maswali Yaliyoulizwa Mara Kwa Mara na Majibu yake

1. e-Kijumbe ni nini?

Ni mfumo wa kidigitali unaowezesha wanachama kuchangiana hela kwa ratiba ya mzunguko, kupitia tovuti rasmi www.ekijumbe.xyz, kwa usalama, uwazi, na nidhamu.

2. Nawezaje kujiunga na kikoba?

Tembelea tovuti yetu, jaza fomu ya usajili na ulipie ada ya uanachama 1,000TZS kupitia Airtel Money. Baada ya hapo, utachagua kikundi kulingana na uwezo wako.

3. Je, pesa zangu zinafanyaje kazi?

Michango ya wanachama hukusanywa na e-Kijumbe, na hutolewa kwa mwanachama anayestahili kupokea kulingana na ratiba ya mzunguko.

4. Ninawezaje kujua ni lini nitapokea pesa?

Unaona tarehe yako ya kupokea kwenye akaunti yako ndani ya tovuti, na mfumo huhakikisha kuwa ratiba inatekelezwa kwa usahihi.

5. Nikiwachelewa kulipa, nini hufanyika?

Mfumo hukulipia kwa niaba yako ili kulinda ratiba, lakini utalazimika kulipa kiasi hicho pamoja na riba ya uchelewaji ya 30%.
Mfano: Ukichelewa kuchangia 10,000 TZS, utarudisha 13,000 TZS.

6. Naweza kupata mkopo mkubwa wa hadi kiasi gani?

Ndiyo, unaweza kupata mkopo mkubwa hadi mara 5 ya kiasi unachopokea kwenye mchezo wako.
Mfano: Kama mchango wako ni 10,000 TZS na unapata 100,000 TZS, unaweza kuomba mkopo wa hadi 500,000 TZS.

7. Je, naweza kuacha kushiriki kikobani?

Ndiyo, unaweza kuomba kujiondoa kwa maandishi. Ombi hilo litapitiwa na uongozi wa e-Kijumbe kwa kufuata masharti.

8. Ninawezaje kuongeza nafasi yangu ya kupokea?

Ukishirikisha mtu mpya ajiunge, nafasi yako ya kupokea husogezwa mbele kwa nafasi moja.

9. Je, malipo yangu yanathibitishwa vipi?

Baada ya kuchangia, utapokea SMS ya uthibitisho kutoka E-KIJUMBE kama risiti halali.

10. e-Kijumbe hufaidikaje?

Mapato ya e-Kijumbe yanatokana na:
- Riba ya mikopo inayotolewa kwa wanachama
- Ada ya uanachama inayolipwa mara moja

11. Je, uongozi wa e-Kijumbe unaweza kubadilisha nafasi yangu?

Hapana, nafasi huamuliwa na mfumo kiotomatiki kulingana na usajili na utendaji wa mwanachama.

12. Ninawezaje kufuatilia historia yangu ya malipo?

Inapatikana ndani ya akaunti yako kwenye tovuti. Unaweza kuona tarehe, kiasi, na uthibitisho wa kila malipo.

13. Je, nawezaje kupata mkopo?

Mkopo hupatikana tu katika tarehe yako ya kupokea na iwapo umechangia kikamilifu bila kukiuka ratiba.

14. Je, kuna adhabu kwa kuchelewa kulipa?

Ndiyo, riba ya uchelewaji ni 30% ya mchango wako, kama mfumo utakulipia ili kuendelea na mzunguko.

15. Ninawezaje kujua idadi ya wanakikoba?

Unaweza kuona idadi ya wanachama katika kikundi chako kupitia akaunti yako. Kikundi kinaweza kuwa na wanachama kati ya 5 hadi 365.

16. Ninawezaje kupata msaada wa kiufundi?

Tembelea ukurasa wa mawasiliano au tuma ujumbe kwenye www.ekijumbe.xyz kwenye sehemu ya icon ya live support au whatsapp icon ya kwenye website.

17. Ninapata faida gani nikishirikisha mtu kujiunga?

Unasogezwa mbele kwenye ratiba ya kupokea.
Mfano: Ukiwa namba 15 na ukaleta mtu mpya, unaweza kuwa namba 14.

18. Je, kuna usalama wa pesa zangu?

Ndiyo. Pesa zote zinasimamiwa na e-Kijumbe hadi muda wa kuwasilishwa kwa anayepokea, kulingana na mtiririko wa ratiba ya mchezo wako.

19. Je, nitalipwa moja kwa moja baada ya mzunguko?

Ndiyo, baada ya wanachama wote kuchangia kwa tarehe yako, e-Kijumbe itakuwasilishia kiasi chako kamili.

20. Malipo ya ada ya uanachama na pesa ya kikoba hutumwa wapi?

Zitume kupitia Airtel Money namba 0780799432 [BRAYAN ERNEST]. Hii ni namba rasmi ya e-Kijumbe.

21. Kuna mikopo ya aina ngapi?

🟢 Mkopo mdogo: Mfumo unakulipia mchango ukichelewa, riba ni 30%.
Mfano: Ukichelewa kuchangia 5,000 TZS, unarudisha 6,500 TZS.

🔵 Mkopo mkubwa: Unaweza kuomba mkopo kwenye tarehe yako ya kupokea, riba ni 20% na unarudishwa ndani ya siku 30.
Mfano: Ukikopeshwa 100,000 TZS, utarudisha 120,000 TZS ndani ya mwezi.